Rais Xi Jinping wa China jana ameanza ziara yake nchini Senegal, na sekta mbalimbali za Senegal zimeikaribisha sana ziara hiyo.
Gazeti la Le Soleil la Senegal limetoa toleo maalumu kueleza ushirikiano kati ya China na Senegal. Makala ya mhariri ya gazeti hilo inasema ziara hiyo ya rais Xi Jinping itahimiza maendeleo ya uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili. Ushirikiano katika madini, gesi asili, miundo mbinu na uvuvi utakuwa na fursa nyingi. Pendekezo la China la kuendelezwa uhusiano wa kiwenzi wa kunufaishana pia linalotafutiliwa na Senegal pamoja na nchi nyingine za Afrika.
Mkuu wa chuo cha Confusius cha chuo kikuu cha Dakar Mamadou Fall amesema, licha ya maendeleo ya uchumi, sayansi na teknolojia, sekta ya utamaduni ya China pia inastahili kuigwa. China imewekeza sana katika mawasiliano ya utamaduni, ili watu wa Senegal waweze kufahamu urithi wa utamaduni wa China, na wachina pia wanaweza kuelewa utamaduni wa Senegal.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |