• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa makala kwenye magazeti ya Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-22 20:30:38

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa makala iitwayo "kushirikiana kufungua kipindi kipya cha urafiki kati ya China na Afrika Kusini" kwenye magazeti ya Afrika Kusini, yakiwemo The Sunday Independent, gazeti la The Sunday Tribune, na gazeti la Weekend Argus.

    Rais Xi amesema, mwaka huu ni maadhinisho ya miaka 20 tangu China na Afrika Kusini kuanzisha uhusiano wa kibalozi. Katika miaka 20 iliyopita, nchi hizo mbili zimeungana mkono na kufundishana zinapotafuta njia za maendeleo zinazoendana na hali halisi yenyewe. Katika miaka 6 iliyopita, China na Afrika Kusini zikiwa nchi mwenyekiti wa pamoja wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, zinashirikiana kwa karibu na kuhimiza maendeleo ya uhusiano na ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika. Uhusiano kati ya China na Afrika Kusini umekuwa mfano wa kuigwa wa uhusiano kati ya China na Afrika, ushirikiano wa Kusini na Kusini na ushirikiano wa nchi za soko jipya, pia una umuhimu mkubwa kwa kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa China na Afrika, kujenga uhusiano wa aina mpya wa kimataifa wenye kuheshimiana, haki na usawa na kunufaishana.

    Kwa sasa, Afrika Kusini iko kwenye njia mpya ya ujenzi na maendeleo ya taifa. Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa malengo ya kujiendeleza kiuchumi, kuongeza nafasi ya ajira, kuboresha maisha ya watu na kuhimiza mageuzi ya kijamii. China inapenda kushirikiana na Afrika Kusini kutumia fursa hii ya maadhimisho ya miaka 20 tangu CHina na Afrika Kusini kuanzisha uhusiano wa kibalozi, kuhimiza uhusiano kati ya China na Afrika Kusini uendelee kwa kasi na mzuri zaidi.

    Mwaka huu pia ni maadimisho ya miaka 10 ya mkutano wa viongozi wa BRICS. China inaunga mkono Afrika Kusini kuendesha mkutano huo wa viongozi wa nchi za BRICS, kuzidisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa BRICS, kuimarisha ushirikiano na mshikamano wa nchi za BRICS, kuzisaidia nchi tano za BRICS kujiendeleza kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako