• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Senegal wahudhuria hafla ya kukabidhi wa uwanja wa mieleka

    (GMT+08:00) 2018-07-23 07:10:23

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Senegal Bw. Macky Sall jana walihudhuria hafla ya kukabidhi uwanja wa mieleka wa taifa uliojengwa kwa msaada wa China.
    Rais Xi na mkewe Bibi Peng Liyuan walipokelewa na rais Sall na mkewe Bibi Marieme kwenye uwanja huo ulioko kitongoji cha Dakar, ambako picha kubwa ya marais hao wawili ilitundikwa kwenye mlango wa kuingilia.
    Kwenye hafla hiyo, rais Xi alimkabidhi ufunguo wa dhahabu wa mradi huo rais Sall. Baada ya hapo, waliangalia maonesho ya mieleka ya kijadi ya Senegali.
    Rais Xi amesema, mradi huo wa uwanja wa mieleka wa taifa ni ishara ya urafiki mkubwa kati ya watu wa China na Senegal. Aidha akiisifu Senegali kama nchi ya utamaduni, rais Xi amesema China inataka kushirikiana na nchi hiyo kufanya juhudi kulinda na kuenzi utamaduni wa jadi, ili kuhimiza mawasiliano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako