• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wenye hasira wawaua wanajeshi watatu kwenye mpaka wa Uganda na DRC

    (GMT+08:00) 2018-07-23 09:09:04

    Jeshi la Uganda limesema wanajeshi wake wameuawa na watu wenye hasira kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

    Akiongea na Shirika la habari la China Xinhua, msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire, amesema watu wenye hasira kutoka nchi hizo mbili wamewaua wanajeshi waliokuwa kwenye forodha ya Vura kaskazini magharibi mwa wilaya ya Arura, ambayo ipo mpakani na DRC wakiwashuku kuwa ni majambazi wenye silaha Jumamosi usiku.

    Amesema kwa sasa uchunguzi unaendelea ili kujua mazingira ya vifo hivyo. Kwa mujibu wa habari polisi wamewakamata washukiwa wanane ili kusaidia uchunguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako