• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watatu wenye silaha wauawa baada ya kuvamia jengo la ofisi za serikali nchini Iraq

    (GMT+08:00) 2018-07-23 19:00:53

    Vikosi vya Kikurdi vimewaua watu watatu waliokuwa na silaha ambao walivamia jengo la serikali katika mji wa Erbil ulioko mkoa wa kaskazini wa Erbil nchini Iraq mapema leo.

    Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutajwa kimesema, vikosi hivyo vimedhibiti tena jengo la serikali lililoko mjini Erbil baada ya kuwaua magaidi hao, pia vikosi hivyo vimefanikiwa kuwaokoa watu watatu ambao walichukuliwa mateka na washambuliaji hao.

    Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo, hata hivyo vikosi vya usalama vinasema wapiganaji wa kundi la IS wanaweza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako