• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Rwanda zaahidi kuandika ukurasa mpya wa uhusiano wa pande mbili

    (GMT+08:00) 2018-07-23 23:08:07

    Rais Xi Jinping wa China aliyeko ziarani nchini Rwanda na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame wamekubaliana kuinua zaidi ushirikiano wa pande mbili kwa lengo la kuwanufaisha zaidi watu wa China na Rwanda na Afrika kwa ujumla.

    Marais hao wamepongeza kukua kwa uhusiano wa pande hizo mbili uliodumu kwa zaidi ya miaka 47 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.

    Rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na Rwanda kubadili uhusiano wa jadi wa kirafiki na kuwa wenye manufaa kwa nchi hizo mbili na watu wake, na pia kufungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa kirafiki wa nchi hizo. Rais Xi pia amepongeza ushiriki wa Rwanda katika ushirikiano wa kimataifa chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kushawishi uwekezaji zaidi wa kampuni za China nchini Rwanda ili kusaidia kuendeleza sekta ya viwanda nchini humo.

    Rais Xi aliwasili Rwanda jana kwa ajili ya ziara ya kiserikali, ikiwa ni ziara ya kwanza kwa rais wa China nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako