• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame

    (GMT+08:00) 2018-07-24 07:04:30

    Rais Xi Jinping wa China jana amefanya mazungumzo na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mjini Kigali. Viongozi hao wawili wamesifu mafanikio ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zao yaliyopatikana katika miaka 47 iliyopita tangu zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, na wamekubaliana kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa nchi zao.

    Katika mazungumzo yao, rais Xi Jinping amasema China inapenda kushirikiana na Rwanda katika kuufanya urafiki kati ya pande mbili uwanufaishe wananchi wa nchi zao. Rais Kagame amesema China ni mwenzi wa kuaminika kwa nchi za Afrika, na kuna umuhimu mkubwa kwa Rwanda na Afrika kuendeleza uhusiano wa kirafiki na China. Rais Kagame amesema,

    "Ninasifu uhusiano wa wenzi na China pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na China katika maendeleo ya uchumi na jamii ya Afrika. Tunatarajia kuwa Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi wa tisa mjini Beijing utatupatia nafasi nzuri zaidi za kuhimiza ushirikiano na kuwanufaisha zaidi wananchi wa nchi hizo mbili."

    Wakikutana na wanahabari baada ya mazungumzo, Rais Xi amesema rais Kagame wa Rwanda amebadilisha maoni naye juu ya uhusiano kati ya nchi mbili, Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika pamoja na masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, na kufikia makubaliano mengi. Rais Xi anasema,

    "China na Rwanda zina fursa muhimu za kuimarisha ushirikiano wa kirafiki, pande zote mbili zinapaswa kuendeleza uhusiano na kuongeza kiwango cha kuaminiana kisiasa kwa mtizamo wa kimkakati na wa muda mrefu. Tunaungana mkono katika kuendeleza nchi kwa njia inayolingana na hali halisi ya nchi zetu, na kuendelea kuelewana na kusaidiana katika masuala yanayohusisha maslahi makuu ya upande mwingine na mausula mengine makubwa tunayoyafuatilia. Tumekubaliana kwamba nchi zetu zinapaswa kuunganisha kwa pamoja mikakati yetu ya maendeleo, na kupanua ushirikiano wa kiutendaji kwenye sekta za uwekezaji, biashara, miundombinu na nyinginezo, ili kuinua zaidi kiwango cha ushirikiano na kuwanufaisha zaidi wananchi wa pande mbili. China inaikaribisha Rwanda kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'".
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako