• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China awasili Afrika Kusini kwa ziara ya kiserikali

    (GMT+08:00) 2018-07-24 08:34:40

    Rais Xi Jinping wa China amewasili Pretoria na kuanza ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini.

    Akitoa salamu za dhati na matumaini mema kwa serikali ya Afrika Kusini na wananchi wake kwa niaba ya serikali na watu wa China, Rais Xi amesisitiza kuwa katika miaka 20 iliyopita tangu China na Afrika Kusini zianzishe uhusiano wa kibalozi, uhusiano wa nchi hizo umeendelezwa katika nyanja mbalimbali, na ngazi yake imeinuka kutoka uhusiano wa kiwenzi, uhusiano wa wenzi wa kimkakati na hadi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote. Ameeleza matumaini yake kuwa wakati wa ziara hiyo, atabadilishana maoni kwa kina na rais Cyril Ramaphosa kuhusu uhusiano kati ya pande mbili, mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba mjini Beijing na masuala ya kimataifa na kikanda wanayofuatilia kwa pamoja, ili kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika Kusini katika zama mpya na kuwanufaisha wananchi wa nchi zao.

    Rais Xi amesema anatarajia kujadiliana na viongozi wa nchi za BRICS, nchi za Afrika, nchi nyingine zinazoibuka kiuchumi na zile zinazoendelea, na kuinua umoja na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea kwenye kiwango kipya, ili kutoa mchango zaidi kwa amani na maendeleo ya dunia.

    Rais Xi amewasili Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara nchini Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako