• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yasema wapiganaji 87 wa al-Shabaab waliuawa katika shambulizi lililoshindwa dhidi ya kambi ya jeshi

    (GMT+08:00) 2018-07-24 10:09:02

    Naibu waziri wa habari wa Somalia Bw. Adam Isak amesema wapiganaji 87 wa kundi la al-Shabaab wameuawa kwenye mapambano na jeshi la serikali katika eneo la Bar-Sanguni baada ya kushindwa kuishambulia kambi ya kijeshi kwa mabomu yaliyotegwa kwenye gari.

    Bw. Isak pia amesema hivi sasa vikosi vya serikali vinadhibiti kikamilifu kambi hiyo.

    Kamanda wa jeshi la Somalia katika eneo hilo Bw. Mukhtar Abdi amethibitisha kuwa wanajeshi wanne wa serikali wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa katika mapigano hayo na wapiganaji wa Al-Shabaab, na kukanusha madai ya wapiganaji kuwa wamedhibiti kambi na kuwaua wanajeshi 27 wa serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako