• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ghana amteua mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2018-07-24 10:09:29

    Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana amemteua mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Washauri Mabingwa wa Masuala ya Uchumi IEA Bw. Jean Adukwei Mensa kuwa mwenyekiti mpya ya Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo.

    Uteuzi huo umekuja baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bibi Charlotte Osei kuondolewa kufuatia pendekezo lililotolewa na kamati iliyoanzishwa kuchunguza malalamiko tofauti dhidi ya Bibi Charlotte Osei na maofisa wengine wa ngazi ya juu wa Tume hiyo.

    Kamati hiyo ilipendekeza kuondolewa kwao kutokana na sababu za mienendo mibaya na kukosa ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako