• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ANC yaahidi kuimarisha nafasi ya Afrika Kusini kwenye BRICS

    (GMT+08:00) 2018-07-24 10:28:30

    Chama tawala cha Afrika Kusini (ANC) kimeahidi kulinda na kuimarisha nafasi ya nchi katika kundi la BRICS.

    Kabla ya mkutano wa 10 wa kilele wa BRICS utakaofanyika huko Johannesburg kuanzia tarehe 25 hadi 27 mwezi huu, ANC imesema mkutano huo utakuwa muhimu, kwa kuwa kundi hilo linatimiza miaka kumi tangu lianzishwe.

    Msemaji wa ANC Bw. Pule Mabe amesema ANC inapaswa kutumia kundi la BRICS kuhimiza ajenda ya kimataifa ya maendeleo, na kwamba ina uhakika kuwa BRICS ni ufunguo wa baadhi ya changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoikabili Afrika Kusini kama vile umaskini, ukosefu wa ajira na ukosefu wa usawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako