• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na India zapenda kushirikiana na nchi za Afrika kupata maendeleo ya pamoja

    (GMT+08:00) 2018-07-24 18:53:56

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, China na India zinapenda kuongeza ushirikiano na nchi za Afrika katika sekta mbalimbali, ili kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja.

    Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi jana walifanya ziara nchini Rwanda, na kusaini makubaliano kadhaa ya ushirikiano na Rwanda. Bw. Geng amesema zikiwa nchi kubwa zinazoendelea duniani, China na India ni wenzi wenye nia moja katika kuzidisha ushirikiano na Afrika.

    Bw. Geng pia amesema rais Xi na Bw. Modi wanatarajiwa kukutana wakati wa mkutano wa nchi za BRICS utakaofanyika nchini Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako