• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wananchi wa Afrika Kusini wana matumaini mazuri kutokana na mkutano wa kilele wa BRICS

    (GMT+08:00) 2018-07-24 18:57:05

    Mkutano wa kilele wa kundi la BRICS unatarajiwa kuanza kesho mjini Cape Town, Afrika Kusini, ukiwa na kauli mbiu ya "BRICS barani Afrika: Ushirikiano kwa Maendeleo, Ustawi wa Pamoja na Mapinduzi ya 4 ya Viwanda"

    Wananchi wa huko wameeleza kuwa tukio hilo litakuwa na athari chanya kwa nchi na maisha yao kwa ujumla. Kutokana na nchi hiyo kukabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi zikiwemo ukosefu wa ajira, ukosefu wa usawa na umasikini, baadhi ya wananchi wa huko wanaamini kuwa mkutano huo utashughulika na changamoto hizo.

    Baadhi ya wananchi hao waliozungumza na Shirika la Habari la China Xinhua wamesema, wanaelewa kuwa mkutano huo pia unapaswa kufuatilia mambo yanayotokea ndani ya nchi wanachama na dunia, lakini masuala hayo hayatakuwa na umuhimu kama wasipozungumzia mambo yanayowagusa vijana, kama vile kazi na fursa nyingine baada ya kuhitimu vyuo vikuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako