• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda na China zasaini makubaliano 15

    (GMT+08:00) 2018-07-24 19:20:59

    Rwanda na China zimesaini makubaliano 15 wakati wa ziara ya Rais Xi Jinping nchini humo.

    Rais wa Rwanda Paul Kagame na Xi Jingping walisaini makubaliano hayo mjini Kigali ikiwa ni pamoja na kwenye sekta za biashara, uchukuzi, miundo mbinu, uwekezaji, ngunvu kazi sayansi na teknolojia.

    Aidha China itafadhili upanuzi wa hospitali ya wilaya ya Masaka ambayo ilijengwa kwa msaada wa China na pia kutoka mikopo ya ujenzi wa barabara ya kilomita 66 ya Huye-Kibeho-Munini pamoja na ile ya Bugesera inayoelekea uwanja wa ndege.

    Rais Xi ameitaja Rwanda kama nchi imara na imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

    Sasa Rais Xi yuko nchini Afrika Kusini ambako anahudhuria mkutano wa 10 wa nchi za BRICS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako