• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano kuhusu UKIMWI watoa wito wa kuondoa kikwazo cha ufahamu na kuongeza ukingaji

  (GMT+08:00) 2018-07-24 21:05:12

  Mkutano wa 22 wa siku tano kuhusu UKIMWI wenye lengo la kuondoa kikwazo cha ufahamu na kujenga daraja la kukabiliana na tatizo hilo, umefunguliwa mjini Amsterdam, Uholanzi.

  Mwenyekiti wa shirika la kimataifa la kupambana na UKIMWI, Linda-Gail Bekker, amesema kwenye ufunguzi wa mkutano huo kuwa, hivi sasa vikwazo vikubwa zaidi vya kuondoa UKIMWI ni kukosa ufahamu na sera. Njia pekee mwafaka ni kutoa kipaumbele katika kufuata sera zinazoendana na tafiti za kisayansi, kuwa na fedha za kutosha na ushirikiano kamilifu ili kutimiza lengo la kuondoa ugonjwa huo.

  Habari zinasema, washiriki elfu 15 kutoka sekta mbalimbali watabadilishana maoni kuhusu uvumbuzi wa matibabu na kuzuia ugonjwa huo na sera na hatua halisi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako