• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Afrika Kusini wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-07-24 22:25:24

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo ziarani nchini Afrika Kusini leo huko Pretoria amefanya mazungumzo na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, na kuafikiana kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Xi amesema, China na Afrika Kusini zote ni nchi zinazoendelea, na katika miaka 20 iliyopita  tangu nchi hizo zianzishe uhusiano wa kibalozi zimejitahidi kushirikiana na kupata maendeleo ya pamoja, na kujenga uhusiano mzuri wa kindugu wa kuaminiana, ambao umeleta manufaa halisi kwa nchi hizo mbili.

    Rais Ramaphosa amesema, Afrika Kusini na China zina urafiki wa kijadi, na katika miaka 20 iliyopita, zimefanya ushirikiano wenye ufanisi mkubwa katika nyanja mbalimbali, na uhusiano maalumu wa kirafiki kati yao umewanufaisha wananchi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako