• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Afrika Kusini wahudhuria ufunguzi wa mazungumzo ya ngazi ya juu ya wanasayansi wa nchi mbili

    (GMT+08:00) 2018-07-25 06:49:13

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa jana walihudhuria ufunguzi wa mazungumzo ya ngazi ya juu ya wanasayansi wa nchi mbili mjini Pretoria.

    Rais Xi akihutubia ufunguzi huo amesema China na Afrika Kusini ni jumuiya yenye hatma ya pamoja na jumuiya yenye maslahi ya pamoja kwa ushirikiano wa kunufaishana siku zote. Miradi ya ushirikiano kwenye sekta ya sayansi iliyotolewa katika mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika mwaka 2015, umetekelezwa vizuri na kupata mafanikio makubwa. Ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini kwenye sekta ya uvumbuzi wa sayansi unahimizwa chini ya juhudi za pamoja za pande mbili. Aidha ushirikiano wa teknolojia kwenye sekta mbalimbali pia umepata maendeleo makubwa.

    Rais Xi amesisitiza kuwa ushirikiano wa kisayansi kati ya China na Afrika Kusini na China na Afrika una fursa muhimu mpya. Pande zote zinapaswa kuandaa jukwaa jipya la kufanya uvumbuzi kwa pamoja, kuimarisha mawasiliano kati ya wanasayansi vijana, na kujitahidi kujiunga na mtandao wa uvumbuzi wa dunia, ili kuhimiza ushirikiano wa uvumbuzi wa kisayansi kati ya China na Afrika Kusini uendane na maendeleo ya sayansi ya dunia.

    Rais Ramaphosa amemshukuru rais Xi Jinping kwa kutilia maanani na kuunga mkono ushirikiano wa kisayansi kati ya nchi mbili, pia amesema mazungumzo hayo yameonyesha dhamira ya pande mbili katika kuhimiza ongezeko kupitia uvumbuzi wa teknolojia na uwezo mkubwa wa ushirikiano kwenye sekta hiyo. Amesema China ni mwenzi wa kuaminika wa Afrika Kusini katika ushirikiano wa kisayansi, serikali ya Afrika Kusini inaahidi kuimarisha ushirikiano wa uvumbuzi wa teknolojia ili kukabiliana na mapinduzi ya nne ya viwanda duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako