• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Peng Liyuan ashiriki kwenye sherehe ya kuhitimu ya mafunzo kwa walimu wa shule za chekechea

    (GMT+08:00) 2018-07-25 07:13:23

    Mke wa rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni mjumbe maalumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni UNESCO anayeshughulikia mambo ya kukuza elimu ya watoto wa kike na wanawake Bibi Peng Liyuan, ameshiriki kwenye sherehe ya kuhitimu ya mafunzo ya walimu wa shule za chekechea.

    Bibi Peng Liyuan akihutubia sherehe hiyo amesema, ualimu ni ajira yenye heshima kubwa, na walimu wanapaswa kukumbuka matumaini ya taifa na majukumu wanayoyabeba, kutoa mafunzo kwa maadili na kwa moyo wa upendo, kutafiti masomo bila ya kusita, ili kuwasaidia wanafunzi wakue wataalamu wa hali mbalimbali na kuchangia ustawi wa nchi na maendeleo ya taifa.

    Siku hiyo Bibi Peng Liyuan pia alitembelea shule ya chekechea ya mtaa ulioko kwenye kitongoji cha mashariki mjini Pretoria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako