• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shimo la tabaka la hewa ya ozoni lililoko juu ya bara la Antaktiki limetoweka

  (GMT+08:00) 2018-07-25 09:00:12

  Data zilizokusanywa na satilaiti ya Sentinel-5P ya Ulaya zinaonesha kuwa shimo la tabaka la hewa ya ozoni lililoko juu ya bara la Antaktiki limetoweka Novemba mwaka jana. Tishio la miali ya UV kwa afya ya binadamu limepungua, lakini kama shimo hili litatokea tena au la bado haijulikani.

  Shimo la tabaka la hewa ya ozoni ni moja ya matishio makubwa ya mazingira duniani. Tabaka hili linasaidia kukinga miali ya UV kutoka anga ya juu. Binadamu wakiishi katika mazingira yenye miali mingi kupita kiasi ya UV, watakabiliwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata saratani ya ngozi.

  Idara ya anga ya juu ya Ulaya imesema satilaiti hii pia inachunguza utoaji wa Carbon Dioxide katika Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, na India, na hali ya uchafuzi juu ya miji mikubwa na kwenye njia za ndege.

  Satilaiti hii ilirushwa angani na Idara ya anga ya juu ya Ulaya Oktoba mwaka jana kwa roketi ya Russia aina ya ROCKOT. Inafanya uchunguzi wa vumbi lililotolewa na volkeno, miali ya UV, kemikali kwenye hewa, uchafuzi wa mazingira, ozoni na erosoli hewani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako