• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchafuzi wa chembe ndogondogo hewani utasababisha kufa kwa miti

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:01:20

    Uchafuzi wa chembe ndogondogo hewani utaathiri afya za binadamu, na utafiti uliotolewa hivi karibuni kwenye jarida la Environmental Research Letters la Uingereza unaonesha kuwa kuwepo kwa chembe ndogondogo juu ya majani ya miti kutaongeza hatari ya kufa kwa miti, na kusababisha kupungua kwa eneo la misitu.

    Mimea inarekebisha maji miilini na kuvuta Carbon Dioxide kwa kufunga au kufungua tundu ndogondogo kwenye majani. Utaratibu huo unailazimisha mimea kuchagua kuwa na "kiu" au "njaa". Kufunga tundu hizo kuinasaidia mimea kupunguza mvukizo wa maji, lakini pia kunaizuia isivute Carbon Dioxide. Kufungua tundu hizo kunaisaidia kuvuta Carbon Dioxide, lakini inapoteza maji kwa kasi. Kwa kawaida mimea ina uwezo wa kuhakikisha uwiano huo, lakini uchafuzi mbaya wa chembe ndogondogo hewani unaathiri uwezo huo.

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Bonn Ujerumani wamefanya majaribio ya kuweka miti midogo kwenye vyumba vyenye hewa tofauti. Matokeo yanaonesha kuwa mimea inayoishi kwenye chumba chenye hewa zilizochujwa inatoa maji machache zaidi. Watafiti wanaona kuwa chembe ndogondogo zilizoanguka juu ya majani ya miti zitaongeza mvukizo wa maji, na hatari ya kufa kwa miti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako