• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yatoa orodha yake, Neymar Jr. awekwa kando

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:09:24

    Shirikisho la soka duniani FIFA limemwacha nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2018.

    Katika orodha ya majina 10 yaliyotajwa leo na FIFA nyota huyo hajajumuishwa, hali ambayo imezua mijadala mbalimbali kwa wadau wa soka wengine wakiunga mkono uamuzi wa FIFA na wengine wakipinga kuwa alistahili kuwepo kwenye orodha hiyo.

    Orodha ya wanaume

    Cristiano Ronaldo - Juventus na Ureno

    Kevin De Bruyne - Manchester City na Ubelgiji

    Antoine Griezmann - Atletico Madrid na Ufaransa

    Eden Hazard - Chelsea na Ubelgiji

    Harry Kane - Tottenham na England

    Kylian Mbappe - Paris St-Germain na Ubelgiji

    Lionel Messi - Barcelona na Argentina

    Luka Modric - Real Madrid na Croatia

    Mohamed Salah - Liverpool na Misri

    Raphael Varane - Real Madrid na Ufaransa

    Tuzo hiyo kwa msimu uliopita ilitwaliwa na Cristiano Ronaldo na kuwashinda mpinzani wake Lionel Messi aliyeshika nafasi ya pili na Neymar Jr aliyeshika nafasi ya pili. Kwa upande wa makocha wa kiume tuzo hiyo ilichukuliwa na Zinedine Zidane.

    FIFA pia wametoa orodha ya majina ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo kwa upande wa wanawake, na orodha ya makocha wanaowania tuzo ya ubora kwa mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako