• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa UM asema wote katika ukanda wa Gaza wanatakiwa kurudi nyuma kutoka ukingoni

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:45:36

    Mpatanishaji maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati Bw. Nickolay Mladenov, amesisitiza tena wito wake kwa watu wa ukanda wa Gaza kurudi nyuma, huku akisema wale wanaotaka kuhimiza vita kati ya Israel na Palestina wasifanikiwe.

    Bw. Mladenov amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa baraza la usalama la Umoja huo. Amesema Umoja wa Mataifa na Misri zitafanya juhudi kutekeleza sera ya kinga ili kuhakikisha kuwa Israel na kundi la Hamas wanarudi nyuma kuepusha mapigano ya nne katika muongo mmoja.

    Ijumaa iliyopita wapalestina wanne waliuawa na wengine 210 walijeruhiwa katika mapambano makali kati ya Israel na kundi la Hamas linalotawala Gaza. Mapambano hayo yaliyosababishwa na mauaji ya askari mmoja wa Israel yamekuwa makali zaidi kwenye ukanda wa Gaza tangu mapigano ya yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja yaliyotokea mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako