• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa shirika la WTO asema sasa ni wakati wa kutoa sauti kwa mfumo wa biashara

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:46:02

    Mkurugenzi mkuu wa shirika la biashara la dunia WTO Bw. Roberto Azevedo ameeleza matishio ya kiuchumi na kimfumo yanayoletwa na hali ya wasiwasi inayoongezeka katika biashara ya kimataifa, huku akitoa wito kwa kila mmoja anayeamini biashara kama nguvu itakayoleta mema kutoa sauti kuilinda.

    Bw. Azevedo amesema hayo katika mkutano wa wanachama wote kuwa, nchi wanachama zinafahamu vizuri mgogoro unaozidi katika biashara ya kimataifa. Hali ya wasiwasi inaongezeka, na hatua mpya zinatangazwa mara kwa mara.

    Pia amesema kama itaitwa vita ya kibiashara au la, hakika risasi ya kwanza imepigwa. Hali itakayoendelea kupamba moto italeta changamoto kwa mfumo wa kiuchumi, na italeta tishio kubwa kwa ajira, ukuaji na ufufukaji wa uchumi katika nchi zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako