• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini lakanusha ripoti kuwa spika wa bunge anakaribia kujiuzulu

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:55:32

    Bunge la Afrika Kusini limekanusha habari zililizotangazwa wiki iliyopita na Shirika la habari la Afrika Kusini kuwa spika wa bunge la nchi hiyo Bibi Beleka Mbete, hatarudi kwenye nafasi yake baada ya uchaguzi wa mwaka ujao.

    Msemaji wa bunge la Afrika Kusini Bw Moloto Mothapo, amesema habari hiyo si ya kweli. Amefafanua kuwa, alichosema Bibi Mbete kwenye mkutano wa chama cha ANC kuhusu ardhi ni kuwa, ataendelea kuwahudumia watu wa jimbo lake kwa njia yoyote ile, baada ya uchaguzi wa mwaka 2019. Kauli hiyo ndio ilileta mkanganyiko.

    Bibi Mbete amekuwa akilaumiwa vikali na wabunge wa upinzani wa Afrika Kusini kuwa anamlinda rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma kufanyiwa uchunguzi na kuwajibishwa na bunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako