• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo cha eneo la Afrika cha Benki ya Maendeleo Mapya ya BRICS kimepata maendeleo gani katika mwaka mmoja uliopita

  (GMT+08:00) 2018-07-25 15:25:54

  Benki ya maendeleo mapya ya BRICS ilianzisha kituo chake kwenye eneo la Afrika mwezi Agosti, mwaka 2017, mjini Johannersburg, Afrika Kusini. Je, kituo hicho kimefanya kazi gani na kupata maendeleo gani katika mwaka mmoja uliopita?

  Kituo cha eneo la Afrika cha Benki ya Maendeleo Mapya ya BRICS ambacho ni kituo cha kwanza cha kikanda kilichoanzishwa na benki hiyo, kwa hatua ya mwanzo kililenga kutoa msaada wa fedha kwa miradi kadhaa kuhusu maendeleo endelevu nchini Afrika Kusini, na kilipanuka hatua kwa hatua na kuwa kituo kinachoichukua Afrika Kusini kuwa kiini chake na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika. Bw. Maasdorp amesema, kuanzishwa kwa kituo hicho kutaisaidia benki hiyo kuhimiza utekelezaji wa miradi mbalimbali barani Afrika. Anasema:

  "Madhumuni muhimu ya kuanzishwa kwa kituo hicho ni kuhimiza utekelezaji wa miradi nchini Afrika Kusini. Hivi sasa benki hiyo imeidhinisha miradi mitatu nchini Afrika Kusini, na kituo cha Afrika kimechangia sana utekelezaji wa miradi hiyo. "

  Kituo cha Afrika kiliahidi kuidhinisha mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.5 nchini Afrika Kusini ndani ya miezi 18 wakati kilipozinduliwa, ili kutumiwa katika miradi ya ujenzi wa miundo mbinu, nishati, utoaji wa maji na ushirikiano wa kikanda. Tarehe 20 mwezi Julai, benki hiyo iliidhinisha mkopo wa dola za kimarekani milioni 300 kwa Afrika Kusini, ili kupunguza utoaji wa gesi zinazosababisha ongezeko la joto nchini Afrika Kusini na kukuza sekta ya nishati. Katika miezi miwili iliyopita, benki hiyo pia imeidhinisha dola za kimarekani milioni 200 kuunga mkono miradi ya upanuzi wa bandari ya Durban nchini Afrika Kusini.

  Bw. Maasdorp ameeleza kuwa, miradi hiyo si kama tu imezinufaisha nchi wanachama wa BRICS ikiwemo Afrika Kusini, bali pia umelinufaisha bara zima la Afrika.

  " Mradi ulioidhinishwa hivi karibuni na benki hiyo ni mkopo wa dola za kimarekani milioni 200 kwa Afrika Kusini ambao utatumiwa katika upanuzi wa bandari ya Durban, ambayo ni kituo muhimu cha uagizaji na uuzaji wa bidhaa cha nchi hiyo. Kwa hiyo mradi huo una umuhimu mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya uchumi nchini humo, hata bara la Afrika."

  Bw. Maasdorp ameongeza kuwa, Benki ya Maendeleo Mapya ya BRICS imesaini makubaliano ya ushirikiano na makubaliano mengine ya ushirikiano na Benki ya uwekezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya Asia, Benki ya Dunia pamoja na Benki ya maendeleo ya Afrika, ili kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi hiyo. Baadhi ya miradi ya ushirikiano itahimiza mchanganyiko wa uchumi kwenye bara la Afirka, kuinua kiwango cha maendeleo ya viwanda, na kuisaidia ipate maendeleo endelevu.

  Benki ya Maendeleo Mapya ya BRICS inajishughulisha na maendeleo ya dunia nzima, na inapanga kushirikisha wanachama mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako