• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahudhuria hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na rais wa Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-25 17:48:06

    Rais Xi Jinping wa China amehudhuria hafla ya kumkaribisha na pia kusherehe miaka ya 20 tangu kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili iliyoandaliwa na rais Cyrill Ramaphosa wa Afrika Kusini .

    Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika jana mjini Pretoria, Rais Xi amesema katika miaka 20 iliyopita, uhusiano kati ya China na Afrika Kusini umeendelezwa zaidi, na maendeleo hayo yameonesha kuongezeka kwa ushirikiano kati ya China na Afrika na pia ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea. Pia rais Xi amesisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Afrika Kusini una mustakabali mzuri lakini unahitaji juhudi zaidi, na kwamba pande hizo mbili zinapaswa kusaidiana ili kutimiza maendeleo.

    Rais Ramaphosa amesema, ziara ya rais Xi Jinping imeonesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili umezidi uhusiano wa kawaida, na una maana ya kimkakati. Amesema Afrika Kusini itashirikiana na China kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi hizo mbili, na kuzidisha ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara, sayansi na tekenolojia na utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako