• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Kiwanda cha sukari cha Mumias kufunguliwa tena

    (GMT+08:00) 2018-07-25 19:28:47
    Kiwanda cha sukari cha Mumias kinatarajia kuanza tena oparesheni mapema mwezi ujao baada ya kuongezeka kwa uzalishaji wa miwa.

    Kiwanda hicho kilisitisha oparesheni mwezi Aprili kutokana na kile kilichodai ni uhaba wa miwa.

    Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Mumias Sugar Kennedy Ngumbau alisema kampuni hiyo imezungumza na wakulima kutoka nje ya mji wa Kakamega ili kuleta mazao yao ya miwa katika kiwanda hicho.

    Alisema kuwa kampuni ya Mumias Sugar inatafuta Sh1bilioni moja kutoka kwa hazina ya taifa ili kuwalipa wakulima pamoja na madeni mengine.

    Wakulima wanaidai kampuni hiyo sh700 milioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako