• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Urafiki wa jadi kati ya China na Afrika wazifanya pande hizo mbili kuwa karibu zaidi

    (GMT+08:00) 2018-07-25 20:17:29

    Ingawa China na Afrika ziko mbali, lakini urafiki wa jadi na jumuiya yenye mustakabali ya pamoja zimeunganisha pande hizo mbili kwa karibu. Urafiki huo unaonekana katika ziara za mara kwa mara za viongozi wa pande hizo mbili.

    Kwa sasa, rais Xi Jinping wa China anafanya ziara nchini Afrika Kusini, hii ni mara ya nne kwa rais Xi kufanya ziara barani Afrika katika miaka 5 iliyopita. Vilevile, viongozi mbalimbali wa Afrika pia wamefanya ziara nchini China. Mwezi Machi mwaka huu, marais wa Cameroon, Namibia na Zimbabwe walikuja China. Tunaweza kusema mwaka huu ni mwaka wa Afrika kwa mambo ya diplomasia ya China. Mwezi Septemba, China itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ambapo viongozi wa China na nchi 50 za Afrika watapanga kwa pamoja mustakabali wa kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na maendeleo ya Afrika, na kuendelea kufungua ukurasa mpya wa urafiki na maendeleo ya China na Afrika.

    Kiini cha urafiki kati ya China na Afrika ni "kunufaishana kwa usawa" na "kujipatia maendeleo kwa kunufaishana". Mkutano wa mawaziri wa FOCAC unaofanyika kila miaka mitatu umeonyesha moyo wa kushiriki kwa usawa na pamoja. Msaada wa China kwa nchi za Afrika hauna masharti yoyote, hususan unaonyesha heshima ya China kwa Afrika. Soko la China limefunguliwa zaidi kwa bidhaa za Afrika, na China imesaidia nchi za Afrika kujenga barabara na madaraja ili kuinua kiwango chake cha ubora wa miundombinu, na kujenga maeneo ya viwanda ili kuzisaidia nchi za Afrika kuinua kiwango cha maendeleo ya viwanda. Hayo yote yanaonyesha wazo la "kujipatia maendeleo kwa kunufaishana".

    Kwa sasa, ushirikiano kati ya China na Afrika utaingia kipindi kipya cha historia chini ya kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali za Afrika. Katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya kimataifa, haswa chini ya kuongezeka kwa hali ya kujilinda kibiashara duniani, urafiki huo kati ya China na Afrika unastahili kutunzwa, na ni lazima kulindwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako