• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais wa China yaonesha China inatilia maanani uhusiano kati yake na Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-25 20:28:21

    Rais Xi Jinping wa China anafanya ziara rasmi ya tatu nchini Afrika Kusini, ikiwa ni ishara kuwa China inatilia maanani sana uhusiano kati yake na Afrika Kusini na kutaka kuongeza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Hayo yamesemwa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang, ambaye amesema huu ni mwaka wa 20 tangu China na Afrika Kusini zianzishe uhusiano wa kibalozi, na katika miaka hiyo iliyopita, nchi hizo mbili zimeungana mkono na kuigana uzoefu katika mchakato wa kujiendeleza kwa njia inayofaa.

    Amesema katika ziara hiyo, marais wa nchi hizo mbili wamefikia makubaliano muhimu, na kuafikiana kuongeza mawasiliano ya ngazi ya juu na uaminifu wa kisiasa na kuunganisha mikakati ya maendeleo. Pia wamekubaliana kusukuma mbele ushirikiano halisi, kuongeza mawasiliano ya watu na ushirikiano wa pande nyingi, na kupinga vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako