• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping atoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za BRICS

  (GMT+08:00) 2018-07-26 07:38:48

  Rais Xi Jinping alialikwa kushiriki kwenye Mkutano wa Baraza la viwanda na biashara la nchi za BRICS uliofanyika tarehe 25 na kutoa hotuba muhimu. Rais Xi amesema, hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa yasiyowahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, ambayo yanaleta fursa nyingi pamoja na changamoto zinazozikabili makundi mapya ya uchumi na nchi zinazoendelea. Amesema inapaswa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za BRICS katika mchakato huo wenye mabadiliko ya muundo wa kimataifa, kujiendeleza na kupata maendeleo mapya katika mwongo wa pili wenye mafanikio mazuri.

  Rais Xi akitoa hotuba ya "kufuata mkondo wa wakati na kutafuta maendeleo ya pamoja", amesema mwongo ujao utakuwa kipindi chenye umuhimu mkubwa zaidi cha mabadiliko kwa msukumo wa ukuaji wa uchumi na muundo wa kimataifa, pia ni kipindi ambacho utaratibu wa usimamizi wa dunia utaundwa upya. Kwa hiyo nchi za BRICS zinapaswa kufuata mkondo huo wa kihistoria, kutumia fursa za kujiendeleza kukabiliana kwa pamoja na changamoto mbalimbali, ili kutoa mchango wa kiujenzi kwa ajili ya kujenga mahusiano ya kimataifa ya aina mpya na jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, inapaswa kushikilia ushirikiano wa kunufaishana, na kujenga uchumi unaofungua mlango. Anasema:

  "Ufunguaji mlango na ushirikiano ni kanuni za lazima za kuleta maendeleo ya sayansi na teknolojia, pamoja na uwezo wa uzalishaji. Haipaswi kufanya vita vya biashara wala hakuna mshindi katika vita hivyo. Umwamba wa kiuchumi hauvumiliki, kwani utaharibu maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa na pia kusababisha kujiharibia. Badala ya hatua hizo, nchi za BRICS zinapaswa kushikilia hatua ya kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, kupambana kithabiti na hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara, kuhimiza mafungamano ya kiuchumi duniani yawe wazi zaidi, kuwashirikisha na kuwanufaisha watu wengi zaidi, na kutimiza uwiano na maendeleo kwa pamoja. Pia itasaidia masoko mapya na nchi zinazoendelea, hususan nchi za Afrika na nchi zilizo nyuma kiuchumi duniani, kunufaika na mchakato wa mafungamano ya kiuchumi duniani."

  Rais Xi Jinping ameeleza kuwa, kila nchi ina haki sawa ya kujiendeleza kwa kutumia fursa jipya zinazoletwa na teknolojia mpya. Anasema:

  "Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 imetoa mpango wa jumla wa utekelezaji kwa jumuiya ya kimataifa. Nchi za BRICS zinapaswa kuunganisha ajenda hiyo na mkakati wa maendeleo ya nchi zao, kushikilia kupangilia kwa pamoja maendeleo ya uchumi, jamii na mazingira kwa kuzingatia maslahi ya wananchi, ili kuongeza hisia za furaha na mafanikio kwa wananchi".

  Rais Xi pia amesema Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, pia ni sehemu yenye mustakabali mkubwa zaidi wa maendeleo duniani. China inapaswa kuimarisha ushirikiano na Afrika, kuunga mkono maendeleo ya bara hilo, ili kufanya juhudi za kujenga ushirikiano kati ya nchi za BRICS na bara la Afrika kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa ushirikiano kati ya kusini na kusini, na kufanya ushirikiano na nchi za Afrika katika kupunguza umaskini, usalama wa chakula, uvumbuzi, ujenzi wa miundo mbinu na maendeleo ya viwanda, ili kuchangia katika utekelezaji wa Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika.

  Rais Xi pia ana matumaini kuwa nchi za BRICS, Afrika, masoko mapya pamoja na nchi zinazoendelea, zitajiunga na pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" na kunufaika kwa pamoja.

  Rais Cyril Ramaphosa akihutubia mkutano huo pia anafuatilia sana changamoto kubwa zinazoukabili utaratibu wa biashara ya pande nyingi, akisisitiza kuwa nchi za BRICS zinapaswa kulinda kwa pamoja utaratibu huo. Anasema:

  "Tunafuatilia sana kufufuka kwa sera za upande mmoja duniani, hali ambayo hailingani na kanuni za Shirika la biashara duniani WTO. Tuna wasiwasi kuwa hatua hizo zitaleta athari hasi hususan kwa nchi zinazoendelea na makundi mapya ya kiuchumi. Tunapaswa kuendelea kusukuma mbele maendeleo endelevu hususan ongezeko shirikishi. Nchi za BRICS zimetambua bayana kuwa, zinapaswa kuhimiza utaratibu wa pande nyingi wa biashara ulio wazi, shirikishi na wenye kuwajibika ili kutoa mchango muhimu kwenye utaratibu huo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako