• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya CECAFA: Dogo wa Leicester City aitwa Serengeti Boys

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:00:54

    Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limemuita mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Leicester City ya Uingereza, Anthony Starkie kujiunga na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Serengeti Boys.

    Taarifa ya TFF iliyotolewa jana usiku imesema, Starkie anatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa na Leicester City, mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya wakubwa England.

    Atajiunga na Serengeti Boys ambayo inajiandaa kushiriki michuano maalum ya vijana Afrika Mashariki na Kati ijulikanayo kama CECAFA Zonal Qualification.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako