• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakufunzi bora duniani: Guardiola, Zidane na Deschamps kushindania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:01:38
    Aliyekuwa meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa aliyeshinda Kombe la Dunia Didier Deschamps ni miongoni mwa wakufunzi 11 walioorodheshwa kushindania tuzo ya Fifa ya Kocha Bora wa Mwaka 2018 duniani.

    Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate pia yuko kwenye orodha hiyo baada ya kuwaongoza kufika nusufainali Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990.

    Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, Jurgen Klopp wa Liverpool na kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez wameorodheshwa pia.

    Kocha wa timu ya kinadada ya Chelsea Emma Hayes yupo kwenye orodha ya makocha wa kike.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako