• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za BRICS zashirikiana kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi

  (GMT+08:00) 2018-07-26 11:52:36

  Mkutano wa kumi wa viongozi wa nchi za BRICS unaofanyika kwa siku tatu umefunguliwa huko Johannesburg, Afrika Kusini. Uchambuzi uliotolewa na shirika la habari la Reuters umesema, thamani ya jumla ya pato la taifa la mwaka jana kwa nchi tano za BRICS limezidi dola trilioni 17 za kimarekani, ambalo ni aidi ya thamani hiyo kwa Umoja wa Ulaya. Kutokana na hatua za nyongeza za kuongeza ushuru wa kibiashara zitakazoletwa Rais Trump, viongozi wa nchi za BRICS wanatarajiwa kushirikiana kulinda mfumo wa pande nyingi. Hali ya vurugu ya kibiashara duniani inaweza kusaidia kuhimiza nguvu kwenye shirika hilo.

  Kutokana na kukabiliana na fursa na changamoto zinazoletwa na uchumi wa kidigitali wa mageuzi ya nne ya viwanda, pamoja na mvutano wa kibiashara unazoanzishwa na Marekani, hilo ni chaguo la pamoja na nchi za BRICS.

  Viongozi wa nchi hizo kwenye mkutano wa baraza la viwanda na biashara wametoa hotuba wakisema, watatumia fursa ya mageuzi ya nne ya viwanda, kuongeza biashara na uwekezaji ndani ya nchi za BRICS, na kuhimiza biashara huria barani Afrika, ili kuinua ongezeko la uchumi na maslahi kwa umma. Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa nchi za BRICS zinatakiwa kujenga uchumi wa dunia uliowazi, kupambana kithabiti na hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara, na kuhimiza uhuru wa biashara na uwekezaji, ili kuongoza utandawazi wa uchumi kuelekea upande wa uwazi, uvumilivu, maslahi ya kunufaisha pande zote na uwiano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako