• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko uliotokea mjini Beijing ni tukio la usalama wa jamii

    (GMT+08:00) 2018-07-26 18:41:11

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, mlipuko uliotokea mapema leo mjini Beijing ni tukio la usalama wa jamii, na polisi wa China wameshughulikia kwa wakati.

    Habari kutoka polisi ya Beijing zinasema kuwa, leo saa 5 hivi asubuhi, mwanaume mmoja alilipua vifaa vya mlipuko katika makutano ya barabara ya Tianze na barabara ya Anjialou, na kusababisha kujeruhiwa mikono. Polisi walioko karibu na sehemu hiyo walikwenda kushughulikia na kumpeleka hospitalini. Hakuna majeruhi mengine.

    Habari zinasema, mtu huyu mwenye umri wa miaka 26, ni mzaliwa wa mkoa wa Mongolia ya Ndani. Mpaka sasa uchunguzi bado unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako