• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenzake wa Brazil

    (GMT+08:00) 2018-07-26 18:54:23

    Rais Xi Jinping wa China leo huko Jorhannesburg amekutana na mwenzake wa Brazil Michel Temer.

    Rais Xi amesema, uhusiano kati ya China na Brazil umejengwa kwenye msingi wa kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na kunufaishana, ni uhusiano wa kupevuka kati ya nchi kubwa zinazoendelea. Amesisitiza kuwa, China na Brazil zinapaswa kuimarisha uelekezi na uratibu katika ushirikiano na maingiliano katika sekta mbalimbali, kuhimiza uhuru na urahisi wa biashara, na ongezeko la biashara yenye sifa bora kati ya pande hizo mbili. Pia kujitahidi kujadili namna ya kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na mpango wa wenzi wa uwekezaji wa Brazil, kuendeleza ujenzi wa miradi muhimu, kupanua ushirikiano wenye uvumbuzi, na kuzidisha mawasiliano ya utamaduni.

    Rais Temer amesema, Brazil inazingatia sana pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", inapenda kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika biashara, uwekezaji, ujenzi wa miundo mbinu, nishati na sekta nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako