• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asema China itaimarisha ushirikiano wa kiwenzi na India

    (GMT+08:00) 2018-07-27 06:27:15

    Rais Xi Jinping wa China amesema China inapenda kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano wa kiwenzi unaoendelea na India.

    Rais Xi amesema hayo alipokutana na waziri mkuu wa India Bw Narendra Modi kando ya mkutano wa kilele wa 10 wa nchi za BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Huu ni mkutano wao wa tatu ndani ya miezi mitatu iliyopita.

    Rais Xi amesema wamefanya usanifu wa ngazi ya juu kwa uhusiano wa pande hizo mbili katika msingi wa hali ya jumla na muundo unaoendana na wakati, hatua ambayo ni muhimu katika kutumia ipasavyo sekta mbalimbali chanya katika nchi hizo, na kuimarisha dhamira za watu bilioni 2.6 wa nchi hizo, ili kutengeneza nguvu inazoweza kuhimza uhusiano wa pande mbili. Ameongeza kuwa China iko tayari kushirikiana na India kuhimiza mwelekeo mpya wa uhusiano wao uliopatikana tangu mkutano wao usio rasmi uliofanyika mjini Wuhan, mwezi wa Aprili.

    Bw. Modi amesema mikutano mitatu kati yake na rais Xi ndani ya miezi mitatu imeonesha kuwa nchi hizo mbili zinafurahia uhusiaino wao wa ngazi ya juu. Ameongeza kuwa India inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu na China ili kutengeneza nguvu na fursa mpya kwa maendeleo ya muda mrefu ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako