• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asema China itashirikiana na Argentina kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-07-27 06:29:02

    Rais Xi Jinping wa China amesema China inapenda kushirikiana na Argentina kutoa mchango kwa ajili ya kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi na kuboresha uongozi wa kimataifa.

    Rais Xi amesema hayo alipokutana na mwenzake wa Argentina Mauricio Macri kando ya mkutano wa kilele wa 10 wa nchi za BRICS unaofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

    Rais amesema sera za upande mmoja na vitendo vya kujilinda kibiashara vinaongezeka, na masoko yaliyoibuka na nchi zinazoendelea zinakabiliwa na ongezeko la changamoto mbalimbali. Pia amesema China ikiwa ni rafiki mkubwa na mwenzi wa ushirikiano wa Argentina, inapenda kuunga mkono juhudi za Argentina katika kudumisha utulivu wa kiuchumi na kifedha na inapenda kutoa msaada kadiri iwezavyo.

    Rais Macri ameishukuru China kwa msaada muhimu inaotoa kwa Argentina ili kukabiliana na matatizo ya kiuchumi na kutuliza soko la fedha. Ameahidi kuwa Argentina itaimarisha ushirikiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako