• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais Xi na Erdogan wakubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya China na Uturuki

    (GMT+08:00) 2018-07-27 06:30:28

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, jana walikutana kando ya mkutano wa kilele wa 10 wa nchi za BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, na kukubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao.

    Rais Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Uturuki umeendelezwa vizuri, ambapo maendeleo yamepatikana katika ushirikiano wa nyanja mbalimbali. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Uturuki kuupa uhai, na kuhimiza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo.

    Rais Erdogan amesema maendeleo ya uhusiano kati ya Uturuki na China yanaridhisha, na Uturuki inapenda kufanya mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu na China na kuongeza ushirikiano katika sekta ya uchumi na biashara, uwekezaji, ujenzi wa miundombinu, vita dhidi ya ugaidi na usalama, jambo ambalo ni muhimu kwa maendeleo na utulivu wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako