• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Uganda zaahidi kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili

    (GMT+08:00) 2018-07-27 06:31:36
    Rais Xi Jinping wa China amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na wa kunufaishana na Uganda kwenye sekta mbalimabli.

    Rais Xi amesema hayo jana mjini Johannesburg alipokutana na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni kando ya mkutano wa kilele wa 10 wa viongozi wa nchi za BRICS unaoendelea kufanyika nchini Afrika Kusini.

    Rais Xi Jinping amempongeza Bw. Museveni kwa juhudi zake katika kuhimiza maeneleo ya uhusiano kati ya China na Uganda, na China na Afrika kwa ujumla. Amesisitiza kuwa katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepata maendeleo ya kasi. Mikakati ya maendeleo ya nchi mbili inalingana, kuna fursa muhimu kati ya China na Uganda. Ametoa wito kwa nchi mbili zidumishe mawasiliano ya ngazi ya juu, na kuendelea kuungana mkono kithabiti kwenye maslahi na masuala makuu.

    Rais Museveni amesema uhusiano kati ya Uganda na China umeimarika. Ameshukuru misaada inayotolewa na China, na kuridhishwa na maendeleo ya ushirikiano kati ya pande mbili. Amesema Uganda inapenda kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji na China kwenye sekta za viwanda, ujenzi wa miundombinu, umeme na nyinginezo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako