• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na nchi jirani zakamata tani 17.6 za dawa za kulevya kwenye operesheni ya pamoja

    (GMT+08:00) 2018-07-27 08:56:14

    Polisi nchini China wamesema China na nchi tano jirani zimeshirikiana kwenye operesheni ya pamoja ya kupambana na uhalifu wa dawa za kulevya kwenye eneo la Lancang-Mekong, na kukamata tani 17.6 za dawa za kulevya na washukiwa elfu 15 katika miezi mitatu iliyopita kuanzia Mei.

    Kwenye operesheni hiyo iliyoshirikisha China, Laos, Myanmar, Thailand, Cambodia na Vietnam, polisi pia wamekamata tani 300 za kemikali zinazokusudiwa kutumiwa kutengeneza dawa za kulevya.

    Naibu katibu mkuu wa Kamati ya udhibiti wa dawa za kulevya ya China Bw. An Guojun amesema operesheni hiyo ni sehemu ya mpango wa pamoja wa miaka mitatu wa kupambana na dawa za kulevya katika nchi hizo sita, na operesheni ijayo inatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba hadi Novemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako