• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yazitaka nchi wanachama kulipa ada ya uanachama baada ya kukosa fedha

    (GMT+08:00) 2018-07-27 08:56:52

    Umoja wa Mataifa umezihimiza nchi wanachama kulipa ada ya uanachama kwa wakati na kwa ukamilifu, kutokana na ukosefu wa fedha.

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amesema umoja huo unakabiliwa na ukosefu mkubwa wa fedha kutokana na nchi wanachama kuchelewa kuchangia fedha katika bajeti yake, na kutoa wito wa hatua kuchukuliwa ili kupunguza gharama za matumizi zisizo za wafanyakazi. Imefahamika kuwa mpaka sasa ni nchi 112 kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa zimelipa ada ya uanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako