• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za BRICS wasisitiza kuunga mkono maendeleo ya miundombinu endelevu barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:14:49

    Nchi za BRICS - Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zimetoa Taarifa ya Johannesburg ya Mkutano wa Kilele wa 10 wa nchi za BRICS,

    zikisisitiza tena kuunga mkono maendeleo ya miundombinu endelevu barani Afrika, ikiwa ni pamoja na utatuzi wa suala la nakisi ya fedha katika sekta ya miundombinu.

    Katika taarifa hiyo viongozi wa nchi za BRICS wamekubali umuhimu wa maendeleo ya miundombinu na mawasiliano kati ya nchi za Afrika, pia wamepongeza maendeleo ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili mindombinu ya Afrika, ambayo maendeleo hayo yanaletwa na Umoja wa Afrika kupitia Uhusiano Mpya wa wenzi wa Maendeleo ya Afrika na Mpango wa maendeleo ya miundombinu ya Afrika.

    Taarifa imeongeza kuwa viongozi wa nchi za BRICS wameunga mkono uwekezaji wa miundombinu, ili kuhimiza maendeleo ya sekta ya viwanda, kutoa nafasi za ajira, kuhakikisha usalama wa chakula, kuondoa umaskini na kutimiza maendeleo endelevu barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako