• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tite asaini mkataba utakaomfanya kusalia timu ya taifa ya Brazil hadi Kombe la Dunia la Qatar

  (GMT+08:00) 2018-07-27 10:24:40

  Tayari makubaliano yamefikiwa, na sasa ni rasmi kuwa kocha wa Brazil, Tite amesaini mkataba mpya ambao utamfanya kusalia katika timu ya taifa ya Brazil mpaka fainali zijazo za Kombe la Dunia nchini Qatar. Brazil iliishia nafasi ya sita katika fainali zilizopita nchini Urusi baada ya kupoteza kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Ubelgiji. Ulikuwa ni mchezo pekee kwa Brazil kupoteza katika fainali hizo. Matokeo mazuri pamoja na nidhamu ya timu aliyoijenga ni sababu kubwa kwa Tite kuongezewa mkataba. Tite hajaonyesha nia yoyote ya kuondoka Brazil kwani havutiwi na soka ya barani Ulaya. Katika fainali tatu zilizopita za Kombe la Dunia pamoja na zile za Copa America, mafanikio makubwa ambayo timu ya Brazil iliyapata ilikuwa ni kufika nafasi ya 4. Mwaka ujazo Brazil watakuwa wenyeji wa Copa America hivyo wanahitaji utulivu ambao utawawezesha kutwaa taji hilo. Wakati Brazil wakitakiwa kujizatiti, timu nyingine hazitakuwa na shinikizo sana bali watayatumia mashindano hayo kama maandalizi kwa ajili ya mechi za kufuzu kuelekea Qatar 2022.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako