• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mohamed Salah akipa nguvu kikosi chake cha Liverpool kuilaza Manchester City 2-1

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:25:00

    Mohamed Salah hakupoteza wakati wowote katika ufungaji wa mabao baada ya Liverpool kutoka nyuma na kuishinda Manchester City 2-1 mjini New Jersy Marekani. Mshambuliaji huyo wa Misri, ambaye alifunga mabao 44 katika mechi 52 msimu uliopita alisawazisha bao lililofungwa na Leroy Sane katika kipindi cha pili dakika moja baada ya kuingia kama nguvu mpya mbele ya umati wa mashabiki 52,000. Kichwa chengine cha Salah kilipanguliwa na kugonga chuma cha goli. Bao la penalti la Sadio Mane liliihakilkishia Liverpool ushindi wa kombe la kimataifa. Salah na mshambuliaji wa Senegal Mane walikuwa wanacheza kwa mara ya kwanza tangu mataifa yao kuondolewa katika kombe la dunia katika awamu ya muondoano. Bernado Silva wa Manchester City ambaye timu yake ya Ureno iliondolewa katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali alicheza kwa mara ya kwanza, lakini City bado walikosa huduma za wachezaji 15 walioshiriki katika kombe la dunia Urusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako