• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawataka wafanya kazi wa serikali kusaidia juhudi za kudhibiti bidhaa feki

    (GMT+08:00) 2018-07-27 18:53:30

    Watendaji wote wa taasisi za serikali ya Tanzania waliopo katika mipaka ya nchi, wametakiwa kuwa wazalendo wa kweli kwa kudhibiti bidhaa zisizo na ubora, kuingia nchini ili nchi isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora kwa walaji na watumiaji.

    Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante Ole Gabriel ametoa agizo hilo kwenye eneo la Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya.

    Alisema hayo alipotembelea Kituo cha Pamoja cha Forodha kati ya Tanzania na Kenya, kujionea utendaji kazi na kuona changamoto zinazowakabili watendaji wa taasisi 15 za serikali zilizopo katika kituo hicho.

    Ole Gabriel amesema watendaji wasiwe sehemu ya matatizo, bali wawe sehemu ya kutatua changamoto zilizopo katika kituo cha Namanga ikiwamo kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa na ubora wenye kiwango kinachostahili kwa mlaji na mtumiaji.

    Alisema kuruhusu kuingiza bidhaa zisizo na ubora yaani bidhaa feki ni kuingiza nchi na wananchi wake katika matatizo makubwa na hilo halitavumiliwa kwa mtendaji yeyote aliyefanya hivyo kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine.

    Alisema ili nchi iendelee watendaji wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli, yaani kufanya kazi kwa bidii na kufuata misingi mizuri ya kazi bila ya kushawishiwa na rushwa kwa lengo la kuingiza nchi katika hasara kubwa kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako