• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa viongozi wa BRICS wapata matokeo makubwa

    (GMT+08:00) 2018-07-27 20:27:08

    Mkutano wa kilele wa viongozi wa BRICS uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, umepata matokeo makubwa na kufikia makubaliano mengi ya uchumi na biashara.

    Mkurugenzi wa idara ya kimataifa katika wizara ya biashara ya China Bw. Zhang Shaogang leo amesema, moja kati ya matokeo hayo ni kuwa nchi hizo zimetoa sauti ya pamoja kuhusu kuunga mkono na kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi. Amesema, kwa sasa uchumi wa dunia umeendelezwa kwa utulivu kwa ujumla, lakini wazo la kupinga utandawazi wa uchumi limetokea, ambalo limeleta changamoto kubwa kwa uwekezaji wa biashara na ongezeko la uchumi kote duniani, na nchi mbalimbali zinatakiwa kukabiliana kwa pamoja.

    Amesema nchi za BRICS zikiwa ni nchi zinazoibuka kiuchumi na wawakilishi wa nchi zinazoendelea, zimetoa mchango mkubwa kwa ajili ya ongezeko la uchumi duniani na uwekezaji wa biashara. Chini ya hali hiyo, nchi hizo zina nafasi kubwa na zinapaswa kutafuta uwekezano wa ushirikiano wa uchumi na biashara, na kuinua kiwango cha ushirikiano wa biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako