• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhuru na ukamilifu wa ardhi wa Syria wapaswa kuheshimiwa

    (GMT+08:00) 2018-07-27 20:28:19

    Mjumbe maalum wa China anayeshughulikia suala la Syria ambaye yupo ziarani nchini Syria Bw. Xie Xiaoyan, amesema uhuru na ukamilifu wa ardhi wa Syria vinapaswa kuheshimiwa, na China inapenda kushiriki kwenye kazi ya ufufuaji wa nchi hiyo.

    Bw. Xie amesema hivi sasa, vita ya kusini mwa Syria inakaribia kumalizika. China inatarajia pande zote zitaharakisha kurudi kwenye mchakato wa kisiasa na masuala yanayofuatiliwa zaidi na pande zote.

    Habari zinasema katika ziara hiyo, China na Syria zimefikia makubaliano katika kuendelea kusukuma mbele mchakato wa kisiasa, kupambana na ugaidi, kuwashughulikia vizuri wakimbizi, na kazi ya kujenga upya ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako