• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China awasili Mauritius kwa ziara ya kirafiki

    (GMT+08:00) 2018-07-28 09:11:29

    Rais Xi Jinping wa China jana aliwasili Mauritius kwa ziara ya kirafiki. Akiwa uwanja wa ndege Rais Xi na mkewe, Peng Liyuan, walilakiwa na Waziri Mkuu Pravinda Jugnauth na mkewe, Kobita Ramdanee, na baadaye Bw. Jugnauth alifanya sherehe kubwa ya kumkaribisha.

    Viongozi hao walikuwa na mazungumzo, ambapo rais Xi alisema amehisi urafiki wa kina wa watu na serikali ya Mauritius waliouonesha kwa Wachina wakati walipowasili.

    Amesema China na Mauritius zimefurahia uhusiano wa pande mbili, na kwamba anatarajia kubadilishana mawazo na Jugnauth juu ya uhusiano wa pande mbili na masuala ya kikanda na kimataifa wanayoyafuatilia.

    Akimkaribisha mgeni wake, Bw. Jugnauth amesema ni heshima kumlaki rais wa China na leo ana matarajio makubwa ya kukutana na rais Xi.

    Mauritius ni kituo cha mwisho cha ziara ya rais Xi nje ya nchi baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais mwezi Machi. Alitembelea nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, Senegal, Rwanda na Afrika Kusini. Pia alihudhuria mkutano wa kilele wa 10 wa BRICS uliofanyika Johannesburg.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako