• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hotuba ya rais Xi kwenye mkutano wa kilele wa BRICS yapongezwa sana na waangalizi wa kimataifa

  (GMT+08:00) 2018-07-28 10:03:29

  Hotuba ya rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa 10 wa wakuu wa nchi za BRICS imepongezwa sana na wasomi na waangalizi wa nchi hizo na nchi nyingine.

  Mkutano huo wa kilele wa makundi ya uchumi wa soko yaliyojitokeza hivi karibuni uliofanyika tarehe 25 hadi 27 umekutanisha viongozi kutoka nchi wanachama wake yaani Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini ili kujadili njia za kutafuta maendeleo na ustawi wa pamoja wakati wa changamoto mpya zinazoikabili dunia.

  Macharia Munene, profesa wa mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani nchini Kenya amesema pendekezo la rais Xi la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo tano za BRICS kama vile katika sekta za biashara, uwekezaji, fedha na mawasiliano litasaidia kutengeneza utaratibu wa kiuchumi ulio na haki zaidi duniani.

  Amesema ushirikiano wa usalama wa kisiasa ni sehemu muhimu katika ushirikiano wa BRICS, ndiyo maana mwito uliotolewa na rais Xi ni muhimu katika kuimarisha amani duniani.

  Mhadhiri wa ngazi ya juu katika Chuo Kikuu cha Limpopo nchini Sudan Kusini Shepherd Mpofu amesema mwito uliotolewa na rais Xi wa kulinda kithabiti amani na usalama wa kimataifa pamoja na kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo umetia moyo wakati dunia inakabiliwa na changamoto za kiusalama zinazoongezeka.

  Profesa wa Kituo cha Utafiti wa China na Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia katika Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru nchini India B.R. Deepak amesema rais Xi amekuwa akihimiza "moyo wa BRICS" wa ushirikiao wa kiwenzi katika msingi wa kuaminiana, kuheshimiana na usawa.

  Kwa maoni ya Ronnie Lins, mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti na Biashara cha China na Brazil, sera ya utaratibu wa pande nyingi, mazungumzo na ushirikiano ni njia muhimu kwa nchi za BRICS kuhimiza mahusiano yao. Amesema hivi asasa, nchi tano wanachama wa BRICS wametunga na kutumia utaratibu wa mazungumzo yanaohusisha sekta mbalimbali, hatua ambayo imeziwezesha kutumia majukwaa mbalimbali ya mazungumzo kutafuta ufumbuzi na kushughulikia matatizo, na kutoa mfano wa uhusiano wa kiwenzi wa kimataifa wa ushirikiano wa kutafuta ushindi na manufaa kwa pamoja.

  Katika hotuba yake, rais Xi alipendekeza kutafuta uwekezaji wa kufanya ushirikiano wa BRICSPlus ndani ya Umoja wa Mataifa, kundi la G20 na mifumo mingine ili kutafuta maslahi mengi ya pamoja na kutengeneza nafasi za maendeleo kwa masoko yaliyojitokeza hivi karibuni na nchi zinazoendelea ili kuchangia zaidi amani na maendeleo ya dunia kwa kupitia uhusiano mpana wa kiwenzi.

  Maoni yake hayo yameafikiwa na wataalamu wengi, ambao wameona kuwa muundo wa BRICSPlus utasaidia kuleta umoja wa nchi zinazoendelea na kujenga utaratibu wa kimataifa ulio sahihi na wenye haki zaidi.

  Mtaalamu wa Kituo cha Utafiti wa Mashariki ya Mbali cha Taasisi ya Sayansi ya Russia Basily Kashin amesema pendekezo hilo la rais Xi ni muhimu na kwamba China inafanya juhudi za kutengeneza utaratibu wa pande nyingi ikiwemo BIRCS Plus.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako