• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko la China ni fursa ya dunia

    (GMT+08:00) 2018-07-28 16:45:11

    Maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchini China yatafunguliwa huko Shanghai. Hadi kufikia sasa, kampuni zaidi ya 2800 kutoka nchi na maeneo 130 zimeandikishwa kushiriki kwenye maonesho hayo. Inakadiriwa kuwa zaidi ya wanunuzi laki 1.5 watashiriki kwenye maonyesho hayo. Imefahamika kuwa zaidi ya 30 ya kampuni za nje zimeandikishwa mapema, na kushiriki kwenye maonyesho ya pili ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchini China yatakaofanyika mwaka 2019.

    Maonesho hayo yanayoendeshwa na serikali ya China yanavutia wafanyabiashara duniani. Hivi sasa uchumi wa dunia unaathiriwa na kujilinda kibiashara, kila kampuni inataka kuvunja vikwazo na kutafuta fursa mpya. Kwa watengenezaji duniani, China ina soko la wateja bilioni 1.4, na serikali ya China inaunga mkono biashara huria na kutoa urahisi kwa uwekezaji, vilevile inafungua zaidi mlango wake nje. China imechukuliwa kuwa fursa nzuri zaidi katika dunia nzima.

    Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni kwenye mkutano wa viwanda na biashara wa nchi za BRICS amesisitiza kuwa, China itaendelea kufungua mlango, kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuimarisha ulinzi wa haki miliki za ujuzi, kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka nje, kuendelea na ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kutengeneza fursa mpya kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi mbalimbali na utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako